Tarehe 18 Machi 2026, Mheshimiwa Meja Jenerali Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri, akiambatana na watendaji wake wawili, alifanya ziara rasmi katika makao makuu ya ofisi za kampuni ya Elsewedy Electric jijini Cairo.

Ziara hiyo ilikuwa na azma ya kukutana na uongozi wa kampuni hiyo, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kufuatilia maendeleo ya uwekezaji wa kampuni hiyo nchini Tanzania.

Lengo la Ziara ilikua ni                                             
(i) Kujadili maendeleo ya uwekezaji wa kampuni ya Elsewedy Electric nchini Tanzania na kutambua changamoto zinazokabili uwekezaji wa kampuni hiyo;

(ii) Kuangalia fursa mpya za uwekezaji ikiwemo miradi ya miundombinu na utalii.