Tarehe 29-03-2026 Mhe. Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
nchini  Misri Mej Jen. Richard M.Makanzo alikutana na Mhe. Lt.  
Gen. Eng. Kamel Alwazeer, Naibu Waziri  Mkuu wa Maendeleo ya  
Viwanda na Waziri wa Uchukuzi katika ofisi yake iliyopo katika Mji  
Mpya wa Serikali (NAC).


Dhumuni la kikao hicho ni juhudi za dhati za Mhe. Balozi za  
kuhakikisha kuwa anatekeleza na kufuatilia masuala mbali mbali ya  
ushirikiano katika sekta ya uchukuzi ikiwa ni sehemu ya kuimarisha  
diplomasia ya Uchumi.

 

Katika yaliyojiri kwenye kikao kilichowakusanya wawili hao ni  
pamoja na; 
Utayari wa Serikali ya Misri katika kuanzisha mradi wa  
“Shipping line” itakayotoa huduma baina ya bandari ya Safaga ya  
nchini Misri na Bandaari ya Dar es  Salaam. Mradi wa “Logistic  
Centre” katika eneo lilolo karibu na bandari ya Dar es Salaam.  
Kubadilishana uzoefu na utaalamu katika sekta ya usafirishaji na  
mradi wa upanuzi wa bandari ya Da es Salaam.

 

Kwa upande wake Mhe. Balozi alimuhakikishia Mhe. Al Wazeer kuwa  
Tanzania iko tayari kufanya majadiliano na Serikali ya Misri  
kuhusu miradi hiyo. Aidha, alibainisha kuwa Bandari ya Dar es  
Salaam ni moja ya bandari muhimu katika Afrika Mashariki, kwani  
inahudumia takribani asilimia 90 ya biashara ya ndani ya Tanzania  
ambapo huzingatiwa kuwa ni bandari muhimu kwa biashara katika eneo  
hilo.

 

Katika kuhitimisha kikao hicho. Mhe. Balozi aliwasilisha salamu  
kutoka kwa Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Uchukuzi wa  
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusisitiza kuwa Tanzania ipo  
tayari kwa ushirikiano kwa ajili ya maendeleo ya mataifa hayo  
mawili.