Katika hatua za kuendeleza sera ya kupata wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nje, Mhe Dkt. Emmanuel J.Nchimbi Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri siku ya tarehe 05/07/2022 alifanya ziara nje kidogo na jiji la Cairo ya kutembelea kiwanda cha Abu AUF kinachomilikiwa na mfanyabishara Bw. Mohamed Auf chenye kujihusisha na uuzaji wa mazao ya nafaka na viungo. Hii ikiwa ni mojawapo ya juhudi za Mhe. Balozi ya kutafuta masoko ya bidhaa na mazao mbali mbali.
Aidha, katika mazungumzo yao Bw. Mohamed Auf alionesha nia yake madhubuti ya kutembelea Tanzania na kuangalia fursa zilizopo kwa ajili ya kununua zao la koroshona kahawa kwa wingi kutoka nchini Tanzania.



