Tarehe 28 Septemba 2026, Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mhe. Maj. Gen. Richard M. Makanzo, alishiriki briefing maalum ya UNIFIL iliyofanyika Beirut, Lebanon, kwa Mabalozi na wawakilishi wa nchi zinazochangia vikosi katika UNIFIL.
Kikao kiliongozwa na Maj. Gen. Diodato Abagnara, Force Commander and Head of Mission of UNIFIL, na kilijadili hali ya usalama kusini mwa Lebanon, utekelezaji wa majukumu ya UNIFIL hadi mwisho wa mwaka 2026, pamoja na mpango wa orderly and safe drawdown and withdrawal wa vikosi kuanzia Januari 2027.
Mhe. Balozi alifuatana na Mwambata Jeshi na Mwambata Fedha wa Ubalozi wa Tanzania, Cairo. Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazochangia vikosi katika UNIFIL.
